Alhamisi , 23rd Apr , 2015

Chama cha walimu Tanzania (CWT) hakijakubaliana na kanuni inayo tumika kukokotoa pensheni za wastaafu na kuwa wastaafu wanapata pesa kidogo wanapostaafu.

Makamu wa rais CWT Honoratha Chitanda.

Akizungumza katika uchaguzi mkuu wa chama hicho mkoa wa Njombe makamu wa rais CWT Honoratha Chitanda amesema kuwa chama hicho hakikubaliani na pesa zinazotolewa kwa walimu hapa nchini kwa kuwa ni ndogo ukilinganisha na pesa wanazo katwa.

Amesema kuwa siku ya leo wanamkutano baina yao na TUCTA ambao utahusisha vyama vyote vya wafanyakazi hapa nchini na kuwa watazungumza suala hilo la kanunu ya ukokotozi wa pesa za wafanyakazi.

Amesema kuwa kwa walimu ni wengi kulikoki sekta yoyote hapa nchini lakini wa pesa wanayo ipata baada ya kufanyiwa ukokotozi wanapata pesa kidogo za kuendesha maisha yao na kuisha maisha mabovu baada ya kustaafu.

Aidha ametumia fulsha hiyo ya usimamizi wa uchaguzi huo wa CWT mkoa kwa nafasi mbalimbali za uongozi kuwataka walimu kuhamasishana kununua hisa katika benki yao ambayo imefunguliwa milango ya kununua hisa kwa watu wote na kuwa wajitahidi kuwa kununua kabla ya kufungwa kwa mlango wa kununua hisa.