Jumatatu , 8th Jun , 2020

Mkurugenzi wa Itifaki na Mafunzo wa CUF Taifa, Masoud Mhina amesema kuwa atahakikisha kipindi chote cha kampeni anakaa Zanzibar ili kuuanika ukweli wa Maalim Seif Sharif Hamad, kuwa hafanyi siasa za ukweli bali anafanya siasa za kudanganya watu kwa maslahi yake binafsi.

Kushoto ni Mkurugenzi wa Itifaki na Mafunzo wa CUF Masoud Mhina, na kulia ni M/Kiti wa chama cha ACT Wazalendo Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad.

Mkurugenzi Masoud ameyasema hayo wakati akiongea na wanachama wa chama hicho, katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, na kusema kuwa watahakikisha wanapita Kijiji kwa Kijiji, Majimbo kwa Majimbo kuuanika ukweli wa Maalim Seif.

Masoud ameongeza kuwa Wazanzibar wanamuamini sana Maalim Seif, wakiamini anawatetea kitendo ambacho si cha kweli bali yupo kwa ajili ya maslahi yake na hivyo wanapaswa kuchuja ukweli na uongo na chama kimedhamiria kuuanika ukweli wote.

"Wanachama wetu mmejenga chama ndani ya miaka 27, leo hii mnakuja kuondolewa na mtu ambaye siyo mkweli kabisa na kama angekuwa mkweli basi mngeona kile anachokisimamia" amesema Masoud.