Ijumaa , 3rd Jul , 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ameongoza mamia ya waombolezaji kutoka ndani na nje ya mkoa wa Morogoro kwenye mazishi ya Chifu wa kabila la Waluguru, Kingalu Mwanabanzi wa 14.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ameongoza mamia ya waombolezaji kutoka ndani na nje ya mkoa wa Morogoro kwenye mazishi ya Chifu wa kabila la Waluguru, Kingalu Mwanabanzi wa 14.

Chifu kingalu wa 14 amefariki dunia siku ya Jumatano ya Julai mosi, katika hospitali ya taifa ya muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuhamishwa akitokea hospitali ya rufaa ya mkoa wa morogoro.

Akitoa rambirambi zake Rais Kikwete amesema kuwa Chifu Kingalu alikuwa msaada mkubwa kwa serikali yake hasa katika usuluhishaji wa migogoro mbalimbali mkoni Morogoro ambapo alikuwa na mchango mkubwa kushinda maafisa wengine wa serikali.

Akizungumza katika mazishi hayo, mlinzi wa marehemu, Haruna Salum amesema kuondoka kwa kiongozi huyo wa kijadi, ni pengo kubwa kwa familia na jamii kwa ujumla.

baada ya maziko ya chifu kingalu, shughuli za kumsimika mrithi wake ambaye ni chifu kingalu mwanabanzi wa 15 zilifanywa,ambapo kwa mujibu wa mila na desturi za ukoo huo, kiti hicho cha uchifu hakikupaswa kuendelea kubaki wazi,

kwa upande wake mkuu wa jeshi la polisi nchini mstaafu, Omary Mahita akieleza namna alivyomfahamu chifu kingalu wa 14 na kwamba alikuwa mhamasishaji mkubwa katika masuala ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira hivyo kuitaka jamii kudumisha mfano huo.