Alhamisi , 5th Mei , 2022

Ushirikiano kati ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo, kiwanda  cha magodoro Vita Foam pamoja na mkuu wa wilaya ya Liwale Judith Nguli umewezesha upatikanaji wa Magodoro 50 yaliyokuwa yanahitajika katika gereza la Wilaya ya liwale ambayo ilikuwa Changamoto ya muda katika gereza hilo

"Hii ilikuwa ni changamoto kubwa kwa wilaya yangu Sina viwanda lakini nimemshirikisha kiongozi wa Temeke leo tumemaliza suala letu niwashukuru sana"alisema Judith Nguli mkuu wa Wilaya Temeke.

Hatua hii ya ushirikiano kati ya Liwale na Temeke  imetajwa kuwa ya mfano wa kuigwa kwa manispaa na halmashauri zingine ambapo wanaweza kuzipatia ufumbuzi changamoto kwa kubadilishana taarifa na kuwashirikisha wadau wa maendeleo waliowekeza kwenye wilaya zao.

"Tulikuwa kwenye kikao kimoja na rafiki yangu kiongozi mwenzangu dada Judith akaniambia changamoto yake nikaipokea nikawambie wadau Temeke leo Magodoro yamepatikana" alisema Jokate Mwegelo - Mkuu wa wilaya ya Temeke.

Awali akipokea magodoro hayo mkuu wa Gereza la Liwale SP Gilbert Sindani amesema  changamoto hiyo imekwisha huku Mkurugenzi Mtendaji wa Vita Foam akibainisha mazingira yanayowekwa kwenye uwekezaji hii Leo yanawasukuma hata wao kuona matatizo ya jamii ni wote.

"Niseme tuu changamoto ya magodoro gereza la Liwale imekwisha na hii imetokana na hawa viongozi kushirikishana changamoto za maeneo Yao" amesema SP Gilbert Sindano - Mkuu wa Gereza la Liwale.

Jokate amesisitiza kuwa wawekezaji wakitumiwa vizuri na viongozi wakashirikiana wanaweza kupunguza sehemu kubwa ya changamoto zinazowakabili wananchi iwe ni za masoko biashara, kilimo na hata utalii.