
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa Chama cha ACT Wazalendo, Abdul Nondo.
Kauli hiyo ameitoa siku za hivi karibuni wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ambapo alisema kuwa yeye anasubiri ridhaa ya wajumbe wa chama chake kama watampa nafasi ya kuwania Ubunge kupitia Jimbo la Kigoma Mjini, basi atahakikisha anaitumia vyema nafasi hiyo na kuendeleza yale mazuri aliyoyaanzisha Zitto Kabwe.
"Chama chetu ni chama ambacho kinaongozwa kwa mfumo wa demokrasia ya wazi, maadili na uadilifu, kujali uzito wa kura ya mtu na kujua ni nani hivi sasa anatakiwa apokeee kijiti, sisi chama chetu hakuna Papa wote ni sawa haijalishi wewe ni kiongozi mkubwa, ama umejiunga leo kwenye chama" amesema Abdul Nondo.
Tazama video hii hapa chini.