
Albert Chalamila
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Mei 15, 2023, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, na kwamba Chalamila amechukua nafasi ya Amos Makalla, ambaye amehamishiwa mkoani Mwanza.
Aidha Rais Samia pia amemhamisha Adam Malima kuwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro, awali alikuwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, na amechukua nafasi ya Fatma Mwassa, ambaye amehamishiwa mkoani Kagera.