Picha kwa hisani ya mtandao.
Akizungumzia kukamatwa kwa Mwalimu, ofisa habari wa chama hicho, Tumaini Makene amesema kuwa Mwalimu ameachiwa jana jioni lakini, mpaka sasa hawajasema walimkamata kwasababu zipi.
Makene amesema awali takribani polisi 10 walifika katika ukumbi wa Mamu mjini humo ambako mkutano huo ulitakiwa kufanyika likotakiwa kufanyika na kukuta maandalizi yakiendelea, ambapo walisitisha mkutano huo kwa maelezo kuwa wameagizwa na William.
“Alikamatwa akiwa anaelekea kwenye kikao cha ndani Mafinga akitokea Kanda ya Nyasa kama mnavyojua tunaendelea na programu ya ujenzi wa chama ikiwemo ya 'CHADEMA ni msingi',” amesema Makene.
Makene ameongeza kuwa, “Polisi watoe taarifa ya tukio hili kuhusu kukamatwa kwa Mwalimu na viongozi wengine".
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire alipotafutwa na www.eatv.tv, kutolea ufafanuzi tukio hilo alipokea msaidizi wake na kueleza kuwa RPC, yupo kikaoni na baadaye baada ya kutafutwa, simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa.

