Jumapili , 20th Jul , 2014

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA imesema kuwa pamoja na serikali kusita kuweka bayana masuala yahusuyo chaguzi za serikali za Mitaa kwa lengo la kushtukiza uchaguzi huo, wao wamejiandaa kushinda chaguzi hizo

Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe.Freeman Mbowe akiongea na awaandishi wa Habari(Hwapo Pichani)

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA imesema kuwa pamoja na serikali kusita kuweka bayana masuala yahusuyo chaguzi za serikali za Mitaa kwa lengo la kushtukiza uchaguzi huo, wao wamejiandaa kwa namna yeyote kushinda chaguzi hizo hata wakishtukizwa.

Akiongea leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe wakati akitoa maazimio ya kamati kuu ya chama hicho pamoja na mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya chama hicho.

Kwa upande Mwingine Mhe. Mbowe akizungumzia mchakato wa katiba mpya amesema viongozi wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA bado wanaendelea na msimamo wao wa kutorejea katika bunge maalum la katiba.