Ijumaa , 8th Jul , 2022

Chama cha Mpinduzi (CCM), kimesema kwamba ajenda ya kupata  katiba mpya sio ngeni, bali ni mchakato endelevu na kwamba sasa ni wakati mwafaka wa kuipata ndiyo maana kimeitaka serikali kuja na namna bora ya kufufua mchakato huo. 

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM , Shaka Hamdu Shaka

Katika ziara yake mapema leo kwenye vyombo vya habari vya IPP vilivyopo Mikocheni Dar es Salaam, ziara iliyolenga kuimarisha mahusiano ya chama hicho na vyombo vya habari, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM , Shaka Hamdu Shaka, amesema kuwa suala la katiba mpya ni moja ya ajenda ambazo Rais Samia Suluhu Hassan, aliomba muda wa kutekeleza , na sasa ni muda mwafaka.
 
"Mimi nilibahatika kuwa mjumbe wa bunge maalum la katiba lililoleta katiba pendekezwa, na mnakumbuka Rais Samia alivyoahidi kwamba apewe muda kuhusu katiba atafanyia kazi, na sasa ni muda mwafaka," amesema Shaka.