Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Hamphrey Polepole.
Akizungumza Asubuhi ya leo ya Machi 11, 2020, na EATV&EA Radio Digital, Polepole amesema kuwa wao kama chama wametekeleza wajibu wao kwa mwanachama mwenzao na kwama chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam kimeshiriki kwa kiasi kikubwa.
"Tunaishukuru CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wametusaidia tangu jana mpaka saa 4:00 usiku, tulikuwa tumekusanya kiasi chote kilichokuwa kinahitajika mahakamani ili kumnusuru ndugu yetu Mashinji, sisi hatuna mashaka na yeye na wala hatutomshikia bango kwamba tulimchangia na hata akiondoka wiki ijayo hatutohuzunika" amesema Polepole.
Dkt Vicent Mashinji pamoja na viongozi wengine wa CHADEMA, katika kesi yao ya uchochezi iliyokuwa ikiwakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana walihukumiwa kulipa faini ama kwenda jela miezi mitano, ambapo faini ya Mashinji ni Milioni 30.

