Alhamisi , 15th Oct , 2015

Chama cha Mapinduzi (CCM),kimesema kimeweka miundombinu na mipango thabiti ya kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi na kufikia malengo waliyojiwekea ikiwa kama watafanikiwa kuingia madarakani na kupunguza matatizo ya vijana.

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Muleba Kaskazini Charles Mwijage wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo. Kulia ni Mgombea Ubunge jimbo la Meleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka

Akizungumza katika mikutano yake aliyoianza mkoani Kagera, Mgombea mwenza wa urais kupitia chama hicho Bi Samia Suluhu amesema kuwa chama hicho kinatambua kuwa vijana ni rasilimali ya taifa na wala sio bomu linalosubiri kulipuka.

Naye mjumbe wa kamati ya kampeni ya chama hicho Bi. Angela Kiziga amesema kuwa serikali ya awamu ya tano itaendeleza kilimo cha ndizi pamoja na kutafuta soko la kimataifa ili kuboresha maisha ya wakulima wa zao hilo.

Naye mbunge anayemaliza muda wake katika jimbo la Muleba Kaskazini, Mh. Charles Mwijage amesema kuwa ukuaji wa teknolojia unawafanya wavuvi kuwa nyuma kimaendeleo hivyo watatoa elimu ya teknolojia ya uvuvi ili waweze kuongeza kipato kutokana na uvuvi bora.