Jumatatu , 13th Jul , 2015

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, Prof. Mussa Assad amesema wataanzisha ukaguzi maalum katika sekta ya mafuta na gesi kubaini uhalali wa mikataba hiyo na kwa kiasi gani itawanufaisha wananchi.

Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Prof. Assad amesema pamoja na ofisi yake kupunguziwa bajeti ya fedha kwa kiasi kikubwa ila ofisi yake itaanzisha ukaguzi maalum kwenye sekta ya mafuta na gesi kuona mikataba ilisainia imezingatia masuala ya maendeleo.

Pr. Assad assad amesema ofisi ya taifa ya ukaguzi kupungizwa bajeti kunakwamisha baadhi ya miradi kutelekelezwa kwa haraka na hivyo kushindwa kufikia maazimio yake kwa wakati.

Kwa mwaka huu wa fedha ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali imepangiwa sh. Bilioni 86 lakini alisema itapatiwa shilingi bilioni 76 pekee kitu ambacho haitatosheleza mahitaji yanayodhamiriwa