Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG Profesa Mussa Asaad
CAG pia amewataka watumishi wa ofisi za ukaguzi kote nchini kutambua wajibu wao kufanya kazi ya ukaguzi inayokidhi viwango vya kimataifa.
Profesa Asaad ameyasema hayo mjini Morogoro wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha iliyoandaliwa na ofisi ya mdibiti na mkuaguzi mkuu hesabu za serikali, ambapo amesema ukaguzi ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Ameongeza kuwa, kuna umuhimu wa kuweka utaratibu wa kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo mara kwa mara ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue ameziagiza wizara idara na taasisi za serikali kuzingatia utekelezaji na ushauri unaotolewa na ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali akisema ushauri huo sio wa hiari ni wa lazima na zaidi wanahitaji kujipanga kudhibiti matumzi mabaya ya fedha za umma kwani wanaoiba rasilimali za taifa nao wamebaini mbinu mpya.