Jumanne , 2nd Apr , 2019

Bunge la Tanzania limemsimamisha Mbunge wa Kawe Halima Mdee kutohudhuria Mikutano miwili ya Bunge kwa kuunga mkono kauli ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof Mussa Assad kwamba.

Uamuzi wa umefikiwa leo baada ya Kamati ya Maadili ya Bunge kupendekeza kutoa adhabu hiyo kwa kile ilichoeleza kuwa ni kumtia hatiani Mbunge huyo na mwenyewe akikiri kuwa alikosea kuunga mkono kauli hiyo.

"Bunge limeazimia kuwa Halima Mdee hatashiriki mkutano huu wa bajeti  na mkutano wa 16 utakaofanyika Septemba na Oktoba, 2019," amesema Naibu Spika Tulia Ackson.

Mapema leo akitoa hukumu juu ya kauli iliyotolewa na CAG, Mwenyekiti wa Kamati ya maadili Emmanuel Mwakasaka alisema, "tumejiridhisha CAG Assad amelidhalilisha Bunge, kamati inamtia hatiani kwa kulidharau Bunge na kudhalilisha shughuli za chombo hiki, kabla ya kupendekeza adhabu, tulirejea kesi zilizowahusu RC Paul Makonda na DC Alexander Mnyeti, kamati imependekeza Bunge lisifanye kazi na CAG Prof. Mussa Assad." - Mwenyekiti

Kauli ya Bunge ni dhaifu pia imemuweka hatiani Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema baada na yeye kurudia kauli hiyo kuwa Bunge ni dhaifu.