Wananchi wakiwa wamejitokeza katika uandikishaji wa daftari la kudumu kwa mfumo wa BVR.
Uandikishwaji bado umeendelea kugubikwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za uchelewaji wa uandikishwaji baina ya mtu na mtu, ambapo kwa masaa mawili wameandikishwa watu 5 katika kitua cha uandikishwaji cha mtaa wa Melinze mkoani hapa.
Robert Mkongwa ni Mmoja ya wakazi wa mtaa wa Melenze amesema kuwa akiwa katika chumba cha uandikishwaji ameshuhuduia zoezi likicheleweshwa na vidole kukataa kusoma katika mashine kIsha kurudia zaidi ya mara tatu.
Baadhi ya wananchi wameonekana wakipeana namba katika moja ya vituo huku, wengine wakiandikana majina ili kulinda nafasi na watu wengi wakiwa wamewahi kutoka saa 11 za alfajili huku kufika majira ya saa moja kamnili watu wakionekana kujipanga katika mistari na idadi yao kuwa zaidi ya watu 40.
Akizungumza na kituo hiki mkoani hapa mratibu wa uchaguzi mkoa wa Njombe Hilmar Danda,amesema kuwa mashine zilizo sambazwa kwa mkoa mzima ni 250 na zoezi rasmi limeanza hii leo na kuendelea na kila kata ambako litatumia wiki moja kukamilika ambapo halmashauri ya mji Njombe zoezi litaanza katika kata za Mjimwema, Yakobi, na Kifanya
Wananchi hao baada ya kuweka majina wameonekana wakiachiana nafasi za kuandikishwa na kuachiana namba za simu ili kuwasiliana foleni itakapo sogea na kuwa wanaenda kuelendelea na kazi zao za kila siku.
Kituo hiki imeshuhudia watu watano wakiandikishwa ndani ya masaa mawili tangu saa mbili asubuhi hadi kufikia majira ya saa nne asubuhi ya siku ya kwanza katika kituo cha Melinze halmashauri ya mji wa Njombe.