Jumatano , 10th Jun , 2015

Zoezi la uandikishaji wa wapigakura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektroniki (BVR) mkoani Mwanza limeigia siku ya pili huku kasi ndogo ya uandikishaji ikishuhudiwa katika baadhi ya vituo vya kuandikishia wapiga kura kutokana na uhaba wa vifaa.

Zoezi la uandikishaji wa wapigakura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektroniki (BVR) mkoani Mwanza limeigia siku ya pili huku kasi ndogo ya uandikishaji ikishuhudiwa katika baadhi ya vituo vya kuandikishia wapiga kura kutokana na uhaba wa vifaa pamoja na wataalam, hali ambayo imelalamikiwa na baadhi ya wakazi wa kata za wilaya ya Ilemela mkoani humo.

Kufuatia hali hiyo baadhi ya wakazi wa mkoa wa Mwanza wameiomba tume ya taifa ya uchaguzi NEC kuongeza idadi ya mashine za BVR pamoja na waandikishaji wenye ujuzi wa kuzitumia mashine hizo.

Mkoa wa Mwanza umepewa mashine 571 za BVR ambazo zitatumika kuandikisha wapiga kura zaidi ya milioni moja na laki nne katika vituo 1500 vya mkoa huo.

EATV imezungukia katika baadhi ya vituo vya kuandikishia wapiga kura na kushuhudia zoezi hilo likiendelea katika hali ya kusuasua licha ya mamia ya wananchi kuitikia vyema zoezi hilo ambalo linawawezesha kupata haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu ujao.

Katika vituo kadhaa vya uandikishaji wa wapiga kura vikiwemo vya kata ya Bugogwa na Sangabuye wilayani Ilemela mkoani Mwanza EATV imeshuhudiwa zoezi hilo likifanyika kwa kasi ndogo na hivyo kusababisha manung’uniko kutoka kwa wananchi kutokana na kukatika mara kwa mara kwa mtandao.

Tags: