Ufanisi huo ni kwa kuzingatia bei, muda, viwango na upendeleo wa zabuni kwa makundi maalum ili kuondokana na mapungufu ya sheria ya ununuzi umma namba 7 ya mwaka 2011.
Katika Kikao cha Hamsini na Mbili cha Mkutano wa Tatu mjini Dodoma, Wabunge mbalimbali wakichangia Muswada huo wamesema itasaidia kuharakisha manunuzi ya bidhaa na huduma za serikali na kuharakisha huduma kwa wananchi huku wakitoa angalizo la kuzingatia ubora
Akiwasilisha Mapendekezo ya Kamati ya Bunge ya Bajeti,Mhe. Hawa Ghasia amesema Muswada huo utasaidia kupunguza mchakato wa ununuzi wa zabuni ikiwa ni pamoja na muda wa mzabuni kuwasilisha malalamiko kutoka siku 28 hadi 7 pamoja na kuongeza upendeleo wa zabuni kwa wazawa pamoja na kupunguza gharama kubwa inayotumiwa na serikali katika kununua magari
Akihitimisha na kujibu hoja mbalimbali za Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango amesema Sheria hiyo itaziba mianya ya upotevu wa fedha za serikali kwa kuwa na Matumizi bora na kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kulinda maslahi ya Wazawa.




