Alhamisi , 17th Apr , 2014

Mwenyekiti wa bunge maalum la katiba Samuel Sitta leo amelitaarifu bunge hilo kuwa kamati ya uongozi ya bunge hilo inatarajiwa kuwa na kikao cha kuzungumzia kitendo cha wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA ) ya kususia Bunge hilo jana jioni,

Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, mheshimiwa Samuel Sitta

Mwenyekiti wa Bunge hilo Mhe. Samwel Sitta alionyesha wazi kusikitishwa na hali hiyo huku mjumbe wa bunge hilo William Lukuvi, naye akionyesha hofu yake juu ya muundo wa muungano wa serikali tatu pamoja na hatua ya wajumbe wanaounda UKAWA kutoka nje ya bunge.

Hata hivyo Bunge hilo liliendelea na mjadala wa kujadili maoni yaliyotolewa na kamati za Bunge hilo bila kuwapo kwa wajumbe hao wa UKAWA.