Ijumaa , 9th Jan , 2015

Jeshi  la  Polisi  Mkoa   wa  Mara limewakamata watu wanne na bunduki  mbili  aina  ya  SMG na  risasi  167 zilizokusudiwa kutumika kwa ujangili wa Tembo katika hifadhi ya Serengeti

Silaha zilizokamatwa

Jeshi  la  polisi  mkoa   wa  Mara kwa  kushirikiana  na  askari   wa  hifadhi  ya  taifa  ya serengeti  limefanikiwa kukamata bunduki  mbili  aina  ya  SMG  na  risasi  167 ambazo  zilikusudiwa  kutumiwa  na  watu   wanne  wanaotuhumiwa  kuhusika  na  vitendo  vya  ujangili  wa  mauaji   ya Tembo  katika  hifadhi  hiyo ya  taifa ya serengeti.
 
Kamanda  wa  Polisi  Mkoa  wa  Mara  Kamishina  msaidizi  Philip  Alex  Kalangi, amesema kuwa polisi  kwa  kushirikiana  na  askari wa hifadhi  hiyo ya  taifa walipata  taarifa kuhusu majangili  hao kuingia katika  hifadhi  hiyo  ya  taifa  kwa  lengo  la  kuua  tembo  kisha  kuweka  mtego  ambao ulishtukiwa  na majangili  kabla  ya  kukimbia  na  kutelekeza  bunduki hizo   mbili, risasi 167   na meno  mawili   ya  tembo.
 
Hata   hivyo  kamanda   huyo   wa   polisi  mkoa  wa   Mara amesema  katika  operesheni ambayo inaendelea  katika   wilaya   za  Musoma, Bunda  na  Serengeti,  askari  wa jeshi  la polisi wamefanikiwa  kuwatia  mbaroni   watu   watano   wanadaiwa  kutumia  funguo bandia  huku  wakivunja  na  kuiba  katika  ghala   la  kuhifadiwa  bidhaa  mbalimbali katika  mtaa  wa  Serengeti mjini Musoma