
Hassan na Michael, walionusurika kuchomwa
Taarifa zimeeleza kwamba vijana hao wameiba mbali kidogo na eneo Mikocheni, na kuanza kukimbia na hatimaye kujikuta mikononi mwa wananchi wenye hasira kali sana, ambapo pia walifanikiwa kujitaja majina yao kwamba ni Hassan na Michael.
Wananchi ambao hawakutaka kurekodiwa wala kujitambulisha majina yao, wamesema kwamba vijana hao wakati wanakimbizwa walianza kuchomoa panga kuwatishia raia waliokua wakiwakimbiza, kabla ya gari moja kuziba njia na kuwezesha vijana hao kuanguka chini na kujikuta mikononi mwa wananchi.