
Bodaboda
Akizungumza na waandishi wa habari Kamishina Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani, ACP Abdil Issango, katika eneo la Vikindu mkoani humo, amesema kuwa operesheni hiyo ni endelevu ndani ya Wilaya ya Mkuranga, kibiti na Rufiji,kwaajili ya kuwakamata madereva wa pikipikiambao hawafuati na kutii kanuni na taratibu za usalama barabarani.
Amesema zoezi hilo linakwenda sambamba na kuwakamata madereva walevi,ambao hawana leseni, pamoja na pikipiki ambazo zinapakia abiria zaidi ya mmoja.
"Ajali nyingi ni bodaboda na kinachowaua ni mwendokasi, ukizingatia barabara zetu hazina miundombinu mizuri kwa kipindi hiki cha mvua, tutakachokifanya ni kuwakamata na kuwalipisha faini" amesema Issango.
Aidha ametoa wito kwa madereva wote wa vyombo vya moto, wazingatie sheria za usalama barabarani kwani mwendokasi unaua.
"Unapolipita gari jingine lazima uwe na uhakika unapopita, inawezekana kule unapopita miundombinu siyo mizuri hivyo unaporudi unaweza ukasababisha ajali" amesema Kamanda Issango.