Ijumaa , 19th Jul , 2024

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond amesema kuwa Tume imeshapata dhamana ya kuanza na skimu 2 za Mwamkulu na Kabage, ambapo ujenzi unaendelea vizuri na kwamba Mheshimiwa waziri wa Kilimo anakuja kuweka jiwe la msingi

pia Tume inaendelea na ujenzi wa Ghala kubwa la kuhifadhi mazao ili kuhakikisha kuwa wakulima hawauzi mpunga badala yake waweze kuuza mchele

Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imewekeza zaidi ya Bilioni 54 katika ukarabati na kuboresha Miundo mbinu ya umwagiliaji katika skimu za Mwamkulu na Kabage ambapo wakulima 2500 watanufaika na kwamba miundo mbinu hiyo itahudumia eneo lenye ukubwa wa hekta 6000 katika kata ya Mwamkulu

Akijibu maswali ya wadau Mndolwa amesema Tume ipo tayari kuendelea kushirikiana na wakulima  kutatua changamoto ikiwepo utengenezaji wa mabirika kwaajili ya kunyweshea mifugo.Amebainisha pia kuwa wizara imejipanga kuanza na ununuzi wa pawa tila 800 kwaajili ya kuwasaidia wakulima Mwamkulu na kwamba Tume inakwenda kuongeza ghala la pili jipya katika kata ya Mwamkulu

Akizungumza kuhusu msimamo na mpango wa serikali, Mndolwa ameeleza wadau kuwa serikali imejipanga kutumia maji ya ziwa Tanganyika kuwawezesha wananchi wa Katavi kupata maji kwaajili ya umwagiliaji, matumizi ya  binadamu pamoja na mifugo; na kwamba serikali haipo tayari kuona wakulima wananyanyasika ndani ya nchi yao