Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo
Kauli hiyo ameitoa hii leo na kusema kupitia fedha hizo Rais Samia pia amewapelekea mradi wa DMDP na tayari wakandarasi wameshaanza kupatikana na kuendelea na kazi katika baadhi ya barabara.
"Ilala ukiingalia unakuta City centre hapa katikati lakini unavyozidi kwenda nje ya mji unaziona zile changamoto za barabara, Rais Samia katuletea zaidi ya bilioni 39 kwa ajili ya barabara jambo ambalo linaenda kujibu kiu kubwa ya adha ya barabara za Wilaya ya Ilala," amesema DC Mpogolo
Aidha katika hatua nyingine DC Mpogolo amesema kuwa katika maendeleo ya jamii serikali imetoa mikopo ya asilimia kumi kwenye halmashauri ya Ilala na fedha ambazo zipo kwenye mzunguko ni zaidi ya bilioni 27 na fedha zilizotengwa kwa mwaka huu wa 2024 ni zaidi ya bilioni 11.