Ijumaa , 23rd Sep , 2022

Ubalozi wa Uswisi kwa kushirikina na ubalozi wa Norway nchini Tanzania, wamesaini mkataba wa zaidi ya shilingi bilioni 3 za Kitanzania kwa ajili ya kuwasaidia vijana wabunifu na wenye vipaji kuweza kujiajiri na kuchangia katika kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.

Mabalozi wakisaini mkataba wa bilioni 3

Akizungumza kwa niaba ya Ubalozi wa Uswisi baada ya zoezi la utiaji saini, Leo Nascher ameeleza kuwa ubalozi utaendelea kuwashika mkono vijana katika kuwajengea uwezo kwenye vipaji na ubunifu ambao wamekuwa wakiufanya, 

Kwa niaba ya Balozi wa Norway Kjetil Schie, amewataka wadau wengine kuungana katika kuwasaidia vijana wenye vipaji na mawazo ya ubunifu, na kuacha kuwakatisha tamaa.

Kwa upande wao vijana wenye vipaji na wanaojishughulisha na sanaa, wamewataka wazazi kubadili mitazamo yao, na kuacha kuwa kikwazo kwa vijana waopenda sambamba, huku wakiomba serikali pia kuwaangalia na kuendelea kuwasaidia.