Alhamisi , 14th Apr , 2022

Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Innocent Bashungwa amesema serikali imetenga shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa soko jipya la kariakoo lililoungua moto tarehe 10 july,2021.

Hayo yamejiri wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya  mapato na matumizikwa ajili ya wizara hiyo, huku serikali pia ikitenga shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 111 za wakuu wa idara.

Kuhusu ujenzi wa barabara tayari ameelekeza wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA kuhakikisha wanawasimamia wakandarasi pamoja na kupata taarifa zao za utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ili kuhakikisha ujenzi unakamilika katika maeneo mbalimbali hapa nchini kurahisisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi.

“Niseme katika mwaka 2022/23 wizara imeongeza shilingi bilioni 4.99 katika mfuko wa jimbo ili kahakikisha maendeleo yanakuwa kwa kasi , kwa sasa mfuko wa jimbo ni bilioni 15 kutoka 11 iliyosimama kwa kipindi kirefu” alisema Bashungwa.

Akihitimisha hotuba yake ya bajeti waziri Bashungwa ameliomba bunge kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi ya kiasi cha shilingi trilioni nane kwa mwaka wa fedha 2022/23