Jumatano , 8th Mar , 2017

Wanawake wametajwa kuwa kundi muhimu katika harakati za kukuza uchumi na kupunguza umaskini katika jamii, kutokana na namna wanavyoshiriki kwa wingi katika shughuli mbali mbali za ujasiriamali.

Sarah Cooke, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na wadau mbalimbali wa masuala ya wanawake, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake, ambapo katika moja ya maadhimisho hayo, baadhii ya wadau wamewapatia wanawake vitendea kazi kwa ajili ya shughuli zao za biashara na uzalishaji mali.

Mmoja wa walioshiriki maadhimisho hayo ni Balozi wa Uingereza hapa nchini Bi. Sarah Cooke, ambaye amesema suala la usawa wa jinsia hususani kipengele cha uwezeshaji wanawake ni la lazima iwapo jamii inataka ipige hatua kimaendeleo.