Biden amesema sababu kubwa ya kujiondoa ni kwaajili ya nchi yake na pia chama chake ili kutoa nafasi ya mtu mwingine atakayegombea katika chama chake na yeye anataka kuwekeza nguvu zaidi ili kumalizia kipindi chake cha miezi minne cha urais kilichobaki.
Biden alikuwa akichuana na mshindani wake wa karibu Bwana Donald Trump toka chama cha Republican ambaye alikuwa mpinzani wake katika uchaguzi uliopita.
Kujiuzulu kwa Biden kunakuja baada ya kuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wafuasi wa chama cha Democratic na viongozi wa chama hicho ambapo walihisi pengine kutokana na umri wake asingekuwa mtu sahihi kwasasa hivyo waliweka shinikizo Biden aachie mbio hizo jambo ambalo Biden alikuwa analipinga lakini hatimaye ameamua kuwasikiliza wafuasi na viongozi wa chama chake.