Balozi wa India nchini Tanzania Debnath Shaw.
wakiongea katika kongamano la siku moja lililofanyika jijini Arusha wadau wa maendeleo na biashara kutoka nchini India akiwemo balozi wa India hapa nchini na Tanzania wamesema hii ni fursa adimu kwa watanzania kuwekeza nchini india .
akifungua kongamano hilo kaimu mkuu wa mkoa wa Arusha Joika Kasunga amesema serikali inafanya kila liwezekalo katika kuondoa vikwazo vya kibiashara baina ya Tanzania na India nchi ambazo zimekuwa na uhusiano wa kibiashara kwa miaka mingi.
Nao baadhi ya washiriki kutoka Tanzania akiwemo Willy Chambulo ambaye ni mdau wa utalii na Sia Marunda ambaye ni afisa mtendaji wa chama cha wafanyabiashara, wakulima na wenye viwanda mkoa wa Arusha wamesema kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa hasa katika kutangaza utalii kwa nchi kama India.
Fursa hii kwa wafanyabishara wa Tanzania wakiwa wanakabiliwa na ushindani mkubwa wa kibiashara hasa katika sekta ya utalii.