
Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
BoT imechukua uamuzi huo kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 33(1) na 33(2) (f) cha Sheria za Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 kutokana na mwenendo usioridhisha wa benki hiyo.
Kutokana na hatua hiyo, kwa mujibu wa sheria sasa imemtemua Bw. Fred Luvanda kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye atasimamia shughuli zote za kiutendaji za benki ya TIB Corpote.
Taarifa ya BoT imesema kuwa hatua hiyo ina lengo la kuboresha usimamizi na utendaji wa mabenki yanayomilikiwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.