Ijumaa , 17th Apr , 2015

Watu 19 wamefariki dunia leo na wengine watatu kujeruhiwa baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kutumbukia mtoni katika eneo la kiwira eneo la ilingodoto, mkoani Mbeya.

Watu 19 wamefariki dunia leo na wengine watatu kujeruhiwa baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kutumbukia mtoni katika eneo la kiwira eneo la ilingodoto mkoani Mbeya.

Akithibitisha kutokea kwa ajili hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amesema basi hilo aina ya Hiace namba T290 ABU lililokuwa likitokea Uyole kuelekea kijiji cha Kiwira ndipo lilipofika eneo hilo la mteremko na likamshinda dereva na kutumbukia mtoni na kupelekea vifo hivyo.

Kamanda Msangi ameongeza kuwa katika ajali hiyo watu 18e walifariki papo hapo na mwingine mmoja alifariki dunia wakati akikimbizwa hosptali kwa ajili ya matibabu zaidi huku watu wakijeruhiwa katika tukio hilo.

Amesema kuwa gari hilo ambalo linafanya safari zake Mbeya mjini lilichukua nafasi ya kubeba abiria kueleka katika gulio la kiwira baada ya kuwepo kwa mgomo wa mabasi aina ya Costa ambayo ndiyo hufanya safari zake huko, ndipo alipowachukua abiria hao kwa kutumia ujanja wa kukwepa askari wa usalama barabarani na kufika eneo hilo lenye mteremko gari kumshinda na kutumbukia mtoni.

Aidha Kamanda Msangi amesema kuwa abiria watu ambao wamejeruhiwa hali zinaendelea vizuri na kuongeza kuwa uchunguzi zaidi unafanyika ili kuweza kuitambua miili wa marehemu katika tukio hilo.