Alhamisi , 11th Jul , 2024

Watu 52 wamenusurika baada ya basi la Kampuni ya Zube lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza kupata ajali katika kijiji cha Njirii Wilayani Manyoni Mkoani Singida.

Kwa Mujibu wa majeruhi ambao ni abiria waliokuwa katika basi hilo wamesema kuwa ajali hiyo chanzo chake ni uzembe wa dereva wa lori lililokuwa likitokea Rwanda kuhama njia yake na kulifuata basi hilo. 

Wamesema kuwa dereva wa basi alijitahidi sana kukwepa lori ili lisigongane uso kwa uso huku pembeni kukiwa na culvert na hatimaye basi hilo kudondoka. 

Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida ili kutoa taarifa kamili zinaendelea.