
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango.
Dkt Mpango ameyasema hayo leo Januari 6, 2020, katika kikao kazi cha Wahasibu wa Serikali wa ngazi za Halmashauri, Taasisi za Umma na Serikali Kuu, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, na kuahidi kuwachukua hatua kali, wale wote watakokiuka maadili ya kazi za Uhasibu huku akiwataka kufichua mianya ya opotevu wa fedha.
Kwa upande wake, Mhasibu Mkuu wa Serikali, Francis Mwakapalila, amesema Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kwa Bara la Afrika kuwa na mfumo imara wa kuimarisha mahesabu ya Serikali.