Jumapili , 8th Mar , 2020

Baba Mzazi wa aliyekuwa muigizaji wa filamu Steven Kanumba, Mzee Kanumba, amefariki Dunia leo Machi 8, 2020, katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, alikokuwa anapatiwa matibabu, msiba upo nyumbani kwake alipokuwa anaishi

Mzee Kanumba na mwanaye Steven Kanumba enzi za uhai wao.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ndugu wa karibu na Baba Kanumba aliyejitambulisha kwa jina la Gideon Simon, amesema kuwa Mzee huyo alikuwa anasumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu sasa.

"Amefariki leo majira ya saa 5 kasoro asubuhi, mimi nilipigiwa simu na Mama ambaye ni mke wake aliyekuwa akiishi naye, kwamba hali ya Mzee imebadilika ghafla na wanampeleka hospitali, lakini baadaye nikapigiwa tena kuambiwa amefariki, msiba upo nyumbani kwake Shinyanga alipokuwa anaishi, na taarifa za mazishi yake zitatolewa baadaye na wanafamilia" amesema Gideon.