Jumapili , 23rd Aug , 2015

Viongozi wandamizi na wanachama wa chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Morogoro akiwemo mwenyekiti wa chama hicho mkoa bwana Magnus Msambira wameamua kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi kadi ya chama hicho na kupokea kadi ya CHADEMA mwenyekiti wa ACT mkoa wa Morogoro Magnus Msambira amesema aliamini ACT ni chama kinachosimamia misingi kumi lakini cha kushangaza viongozi wa ACT wa taifa ndio wamekuwa wa kwanza kuvunja misingi hiyo kwa kuwapora wanachama wake mamlaka na uwezo wa kuchagua viongozi wanaowataka.

Naye mgombea ubunge jimbo la Mlimba wilaya ya Kilombero Susan Kiwanga pamoja na mengine amesema jimbo hilo linakabiliwa na matatizo ya ardhi, kero za walimu, wafanyakazi wa TAZARA pamoja na migogoro ya ardhi ambapo ameitaka tume ya uchaguzi kuongeza vituo vya wananchi kuhakiki majina yao katika daftari la kudumu la wapigakura ili wawe na uhakika wa kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo.