Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri akiwa katika Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Njombe ambapo pamoja na mambo mengine mkuu huyo amezungumzia juu ya haki ya kuishi ya mtoto .
Msafiri amesema anashangazwa na tabia ya wazazi kushindwa kutimiza wajibu wa kuwalinda watoto mda wote jambo ambalo limepelekea baadhi ya watoto kuhatarisha usalama wao .
Mauaji hayo ambayo yameanza kushika kasi Mkoani Njombe tangu Desemba mwaka 2018 yamepelekea watoto tisa kupoteza maisha huku wengine wakishindwa kupatikana mpaka sasa.





