Alhamisi , 4th Aug , 2022

Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amewataka wakandarasi wanaojenga bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika Kata ya Masaka mkoani Iringa, kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kwa wakati uiliopangwa,  ili kusaidia wananchi kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso

Waziri Aweso amesema hayo mkoani Iringa katika ziara ya kutembelea bodi ya maji ya bonde la mto Rufiji, ambapo licha ya kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo wa bwawa ambalo litahudumia wananchi zaidi ya elfu kumi na saba, Waziri amesema ni vyema wakandarasi kuacha visingizio visivyokuwa na ulazima katika kutekeleza miradi ya maji ambayo ina umuhimu mkubwa kwa wananchi

Aidha Waziri Aweso amesema, Wizara ya Maji haitakuwa kikwazo katika kukwamishwa kwa miradi hiyo ambayo inasaidia kutataua changamoto ya huduma ya maji kwa wananchi.