Alhamisi , 11th Mei , 2017

Licha ya Kukiri kuwepo kwa upungufu wa sukari nchini kwa zaidi ya tani laki moja, Serikali imewatoa hofu watanzania na kuwaahidi wananchi serikali inafahamu jambo hilo na tayari imeshaanza kuboresha upatikanaji kulingana na jinsi inavyohitajika

Akiongea leo Bungeni Mjini Dodoma, katika kipindi cha maswali na Majibu kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema kutokana na tatizo hilo serikali imeagiza tani laki moja na 31 na kati ya hiyo tani 80 zimeshaagizwa na tani 35 zimeshaingia nchini ili kukabiliana na tatizo hilo.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa kutokana na kukaribia kwa mwezi Mtukufu wa ramadhani ambapo sukari nyingi inahitajika serikali imeshaweka utaratibu wa kuagiza sukari zaidi ili kufikia malengo umeshaandaliwa.

Mhe. Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara nchi kuacha kupandisha bei ya bidhaa hiyo bila sababu kwani kwa kufanya hivyo kunawaumiza wananchi wakati bidhaa hiyo bado inapatikana kutokana uzalishaji uliopo nchini pamoja na ile waliyoagiza kutoka nje ya nchi.

Msikilize hapa chini majaliwa akizungumza leo bungeni