Jumatatu , 26th Sep , 2022

Mtu mmoja aitwaye Omar Zorwa, amefariki dunia kwa kukatwakatwa na mapanga na mwingine kujeruhiwa, baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya wakazi wa Kijiji cha Kizaru na Kamungendi, wilayani Butiama mkoani Mara katika mgogoro wa kugombea mipaka ya ardhi ndani ya vijiji hivyo. 

Panga

Baadhi ya wanakijiji hao wamezungumzia mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 hivi sasa, ambapo Halmashauri ya Butiama ilimaliza mgogoro huo kwa kuweka mipaka ambayo bado wakazi hao wanaikana kutokuitambua na kuzidi kugombania sehemu ya ardhi hiyo mpaka kuibuka mapigano na kusababisha mauaji.

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa ardhi mkoa wa Mara Agnes Mtutwa, amesema wamejaribu kuutatua mgogoro huo lakini bado wakazi wanauendeleza huku Mkuu wa wilaya ya Butiama akilezea namna tukio hilo lilivyotokea.