Rais wa sasa wa Halmashauri ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma.
Rais wa sasa wa Halmashauri ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma, alikuwa akitarajiwa kun'gatuka lakini viongozi wameshindwa kukubaliana juu ya mtu wa kurithi nafasi yake kuiongoza kamisheni hiyo kuu ya utendaji ya umoja huo wakati wa mkutano wa kilele wa 27 unaofanyika mjini Kigali.
Hakuna mgombea yoyote kati ya watatu waliokuwa wakiwania nafasi hiyo alieweza kujikusanyia wingi wa theluthi mbili ya kura zilizokuwa zikihitajika ili kushinda katika kura hiyo iliopigwa kwa siri.
Kabla ya kupigwa kwa kura hiyo nchi nyingi zilielezea kufadhaishwa kwao kutokana na wagombea hao kutoka Uganda, Botswana na Equatorial Guinea ambao hawajulikani sana kutokuwa na hadhi inayostahiki.
Nchi 28 kati ya 54 za Umoja huo zilijotowa kupiga kura katika duru ya mwisho na kulazimisha kuahirishwa kwa uchaguzi huo na kurefushwa kwa muhula wa Zuma.