Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri nchini (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka (Kushoto)
Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri nchini (ATE), Dkt. Aggrey Mlimuka, ametoa wito huo jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumzia Tuzo ya Mwajiri Bora ya Mwaka 2016, ambazo mgeni rasmi katika tuzo hizo atakuwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
Kwa mujibu wa Dkt. Mlimuka, ufanisi katika uzalishaji unategemea zaidi maelewano mazuri na hivyo ametoa wito kwa waajiri kuhakikisha wanaboresha mazingira ya kazi ikiwa ni pamoja na usalama wa wafanyakazi wao wakati wote wanapokuwa kazini.