Jumapili , 4th Jan , 2015

Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limewazawadia vyeti na fedha askari Polisi wa vitengo mbalimbali wapatao 22 kutokana na utendaji wao mzuri

kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, kamishina msaidizi Mwandamizi wa Polisi Charles Mkumbo

Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limewazawadia vyeti na fedha askari Polisi wa vitengo mbalimbali wapatao 22 kutokana na utendaji wao mzuri uliofanya jeshi hilo kukamata waharifu mbalimbali na kupunguza makosa ya ajali za barabarani katika mkoa huo.

Sherehe za kuwatunuku vyeti askari hao zilianza kwa gwaride ambapo mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Bariadi, Erasto Sima ambaye alimuwakilisha mkuu wa mkoa huo alikagua gwaride hilo.

Akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti hivyo kwa niaba ya Inspekta wa Polisi, kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu, kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Charles Mkumbo amesema kuwa mkuu wa wilaya ya Bariadi Erasto Sima amewataka wananchi wa mkoa huo kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi hususani katika kufichua vitendo mbalimbali vya uharifu.

Pia amewataka kuacha kujichukulia sheria mikononi kwa kutumia mabaraza ya kimila maarufu kama ndaga shida.

Kwa upande wao askari waliotunukiwa vyeti hivyo wamesema wataendelea kufanya kazi yao kwa weledi na kuzingatia maadili ya jeshi la polisi.