Alhamisi , 2nd Jan , 2020

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Flora Adam (23), kwa tuhuma za kumkata mume wake sehemu zake za siri, ambaye ni Askari polisi aitwaye PC Kazimir (28), mkazi wa Shinyanga Mjini, kitendo ambacho kimeelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Picha ya Kisu.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Deborah Magiligimba, amesema kuwa tukio hilo lilitokea Disemba 28, 2019, majira ya saa 6:00 usiku, wakati wakiwa wamelala ambapo ghafla mwanamke huyo alinyanyuka kitandani na kumkata mume wake na kitu chenye ncha kali sehemu zake za siri.

Baada ya tukio hilo Askari huyo, alikimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya Serikali ya Mkoa wa Shinyanga, ambako alilazwa kwa siku mbili na badaye aliruhusiwa.