
Konstebo Samwel Feston Kaziyote
Taarifa ya Jeshi la Polisi ilitolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga, imeeleza kuwa kuwa mnamo Oktoba 02, 2023 majira ya saa 2:15 usiku maeneo ya mtaa wa Mzumbe Forest ya zamani Askari huyo alijipiga risasi kidevuni na kusababisha kifo chake papo hapo.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokea baina yake na mpenzi wake baada ya marehemu kuacha lindo la benki na kisha kuondoka na silaha kwenda nyumbani kwa mpenzi wake huyo na kujipiga risasi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.