Alhamisi , 10th Nov , 2016

Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kimewavua nyadhfa zao mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Tabora Shida Machumu, na mkuu wa usalama barabarani wilaya ya Nzega Thomasi Ngecha kwa kushindwa kutekeleza mkakati wa kupuguza ajali za barabarani

Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim

Akitoa taarifa ya uchunguzi wa ajali iliyohusisha magari mawili na kusababisha vifo vya watu 19 Novemba 6 mwaka huu katika eneo la Nsalala Kata ya Tinde mkoani Shinganga, kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Fortunatus Muslim amesema uchunguzi wa ajali hiyo umebaini makosa yaliyosababisha ni moja wapo na askari wa usalama barabarani kuondoka katika vituo vya kazi.

Kamanda Muslim amesema hatua hiyo imekuja baada ya uchunguzi uliofanyika kumebaini maafisa hao wameshindwa kuwasimamia watendaji walioko chini yao hali ambayo imekuwa ikisababisha ajali za mara kwa mara na kugharimu maisha ya watu wengi.

Aidha ameongeza kuwa Amesema pamoja na kuwavua nyazifa viongozi hao wawili na askari wengine sita wamevuliwa vyeo vyao kwa kosa la kuondoka katika vituo vya kazi kinyume na taratibu.

Ajali iliyotokea Shinyanga

Askari waliovuliwa nyazfa zao ni wale waliokua wamepangwa kazini siku hiyo katika Stendi ya Nzega ni pamoja na Sajenti Charles, askari No 6547 Koplo Heri, WP No.6983 PC Hapi na WP No.7676 Neema na askari wawili waliopangwa kazini eneo la Uchama ambao ni WP No.5791 PC Sesi na WP 7165 PC Aziza wanachukuliwa hatua za kinidhamu na wanaondolewa moja kwa moja katika kikosi cha usalamA barabarani kwa uzembe huo.

Aidha amesema uchunguzi wa Jeshi hilo umebaini kuwa ajali hiyo imesababishwa na mwendo kasi na kuzidisha abiria.

.