Rais wa PAMCA tawi la Tanzania, Dk Stephen Magesa
Akizungumza na East Afrika Radio Rais wa PAMCA Tanzania Dkt. Stephen Magesa amesema kuwa watu laki sita hufariki kila mwaka duniani kwa ugonjwa wa Malaria idadi ambayo imepungua toka Vifo million 2 miaka ishirini iliyopita.
Dkt. Magesa ameongeza kuwa jamii inapaswa kujikinga na malaria kwa kutumia vyandarua vyenye dawa kwani malaria ndio ugonjwa unaoongoza kwa kuua watu wengi duniani hivyo jamii inawajibika kuweka mazingira katika hali ya usafi ili kupunguza mazalia ya mbu wanaoambukiza malaria.
Aidha Dr Magesa ameongeza kuwa PAMCA kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kimataifa za kudhibiti malaria kama Global Fund, WHO na mengine wapo katika mpango wa kuandaa sera, tafiti na mipango ya kupunguza na kuondoa mazalia ya mbu duniani ifikapo mwaka 2030.