Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amesema jeshi la polisi likishirikiana na raia wema wamefakiwa kumkamatwa muuwaji aliyemtaja kwa jina la Elijusi Edward Lyatuu katika eneo la TRA, tarehe moja ya mwezi huu.
Amesema kabla ya mauwaji hayob muuaji huyo ambae ni mwanafunzi wa chuo cha falsafa cha kanisa katoliki mwaka wa tano,kijana Alfred Kimbaa maarufu kama Mandela alikuwa ni rafiki na marehemu lakini, katika hali isiyo ya kawaida wakatofautiana jambo ambalo lilipelekea mtuhumiwa kumnyonga marehemu na baadae kumkata viongo vyake wakiwa hotelini hapo.
Aidha kamanda Libearatu ameongeza kuwa viongo vilivyokatwa vimekutwa vikiwa vimefukiwa katika mto Misheni uliopo Usa River nje kidogo ya mji wa Arusha na kuongeza kuwa ushahidi umekamilika na muda wowote mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Mauwaji haya yalifanyika katika Hotel ya Am iliyopo jijini Arusha na baadae muuwaji huyo kutoweka na viongo mbalimbali vya marehemu ikiwemo kichwa,matiti,mikono na sehemu za siri.