Jumatano , 20th Dec , 2023

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) wamefanya ukaguzi wa kushtukiza ili kubaini kama wananchi wanalipa nauli halali zilizotangazwa na serikali mapema mwezi huu ambapo wamebaini baadhi ya wamiliki na m

Ukaguzi wa tiketi Arusha

na mawakala wa mabasi kuwapandishia nauli wananchi huku mamlaka hiyo ikiwapiga faini kwa kosa la kuzidisha nauli hizo.

Akiongea katika ukaguzi wa nauli hizo mapema leo katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed, amesema wapo katika ukaguzi wa nauli kutokana na malalamiko ya wananchi kupitia simu na mitandao ya kijamii kuhusiana na kupanda kwa nauli.

Ameongeza kuwa kwa sasa ukataji tiketi ni kwa mfumo wa kielektroniki ambapo amesema kuna mifumo mipya inayorahisisha kuangalia bei elekezi ya serikali huku akiwaomba abiria kutumia mifumo hiyo ili kutokuumizwa na nauli kandamizi ambazo zinatozwa na  baadhi ya mawakala na wamiliki wasio waaminifu.

Kwa upande wake Afisa mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA Mkoa wa Arusha Joseph Michael amesema kuwa wamefanya ukaguzi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuangalia utekelezaji wa masharti ya leseni za latra kwa mujibu wa usafirishaji huku akitoa onyo kwa wamiliki na mawakala kutokata tiketi bila kutumia mfumo wa kieletroniki.