
Mmarekani Macon Dunnagan akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii, wakati akipongezwa
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini leo mjini Moshi siku moja baada ya kumaliza kushuka katika Mlima huo Dunnagan ametoa wito kwa Watanzania na wageni kutoka sehemu mbalimbali kuwa na tabia ya kutembelea vivutio vilivyopo nchini Tanzania ili kujionea utajiri na vivutio mbalimbali ambavyo havipatikani sehemu nyingi duniani.
Aidha amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi ikiwa ni pamoja na wanyama wa aina zote wakiwemo Simba Tembo Twiga na Chui pia kupanda Mlima Kilimanjaro.
Balozi Dunnagan ambaye alianza kupanda mlima Kilimanjaro toka mwaka 1999 amesema ataendelea kuiamasisha Dunia kuja kuona maajabu ya vivutio vya Taifa la Tanzania.
Akiongea kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini amesema Serikali itaendelea kutambua michango ya watu wote wanaotangaza utalii wa Nchi wa ndani na wanje akiwemo Macon.
Amempongeza balozi huyo kwa kutoa hamasa kubwa wa watanzania na wamarekani kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya nchi hiyo ambapo amefafanua kuwa Dunnagan alianza kuhamasika kupanda mlima Kilimanjaro mwaka 1967 baada ya kuangalia movi ya “Snow of Kilimanjaro”.