Alhamisi , 14th Apr , 2022

Polisi huko Jijini New York wamemkamata mwanaume mmoja anayetuhumiwa kupiga risasi watu 10 ambao ni abiria waliokua wanasubirua treni katika kituo Cha Brooklyn.

Mtu huyo Bwana Frank James mwenye umri wa miaka 62, alikua amevaa kofia ngumu na nguo maalum kama mfanyakazi wa ujenzi anatuhumiwa kwanza kurusha bomu la moshi Ili watu wasione, Kisha kuanza kurusha risasi.

Msako mkali wa saa 30 ulifanyika na kufanikisha kumtia mbaroni.

Meya wa Jiji la News York Eric Adams alisikika akisema kuwa  "Ndugu zangu wa New York, tumefanikiwa kumpata"

B.James anatarajiwa kufikishwa Mahakamani hii leo kujibu mashtaka yanayohusiana na ugaidi .