Jumamosi , 17th Jul , 2021

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia Grace Mushi (25) kwa tuhuma za kumuuwa aliyekuwa mpenzi wake Khamis Abdallah (25), mkazi wa Mbezi Makabe baada ya kumfungia ndani ya nyumba na kuimwagia mafuta ya petroli na kisha kuichoma moto nyumba hiyo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Muliro Jumanne,

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Muliro Jumanne, na kusema kuwa tukio hilo limetokea Julai 16, 2021, majira ya saa 8:30 usiku na uchunguzi umebaini kwamba wapenzi hao walikuwa na mgogoro mkubwa wa mapenzi.

"Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alijaribu kutoroka lakini kwa kushirikiana na wananchi alikamatwa na uchunguzi wa awali umeonesha kwamba ulikuwepo mgogoro mkubwa wa kimpenzi kabla ya kufanyika kwa tukio hili la mauaji ya kikatili," ameeleza Kamanda Muliro.